Baraza la Mitihani la Tanzania linawajulisha watu wote kuwa mfumo wa Usajili wa Watahiniwa wa Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE), Kidato cha Pili (FTNA) na Mtihani wa Maarifa (QT) 2020 umefunguliwa kuanzia tarehe 22/06/2020 na utafungwa tarehe 05/07/2020. Hivyo, Wakuu wa Shule za sekondari wahakikishe wanakamilisha usajili wa watahiniwa wa Kidato cha Nne (CSEE) na Kidato cha Pili (FTNA) 2020. Aidha, Watahiniwa wa Kujitegemea (CSEE & QT) ambao hawakuwa wamejisajili katika kipindi cha kawaida, wahakikishe wanajisajili kwa kuzingatia utaratibu uliooneshwa kwenye mfumo wa usajili.

Kupata nakala tembelea TANGAZO_LA_USAJILI_WA_CSEE_2020_ baada_ya_ corona_ FINAL