Maadhimisho ya Juma la Elimu (Global Action Week for Education (GAWE) 2022 Mkoa wa Tabora-Wilaya ya Igunga

Kauli Mbiu: Tuwekeze katika Elimu, kwa Elimu Bora

(Financing Education for Improved Learning Outcomes)

Utangulizi

TEN/MET ni mtandao wa kitaifa wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojishughulisha na elimu hapa nchini yenye wanachama nchi nzima wapatao 158. Kwa miaka 15 TEN/MET kwa kushirikiana na serikali na wadau wengine wa elimu nchini tumekuwa tukiitikia wito wa kuadhimisha juma la elimu (Global Action Week for Education-GAWE) hapa nchini. Maadhimisho ya Juma la elimu (GAWE) ni tukio la alama kwa mashirika yasiyokuwa ya kiselikali yanayojishughulisha na elimu duniani kote na uadhimishwa juma la mwisho la mwezi wa nne hadi wa Tano kila mwaka tangu mwaka 2000.

 

Kwa mwaka huu maadhimisho ya Juma la Elimu yatafanyika Mkoa wa Tabora, Wilaya ya Igunga kuanzia tarehe 25 hadi 29 April 2022 Maadhimisho haya yataongozwa na kauli mbiu “Tuwekeze katika Elimu, kwa Elimu Bora na ujumbe “Elimu Kwanza” . Maadhimisho yatahusisha shughuli mbali mbali za kijamii ikiwemo; kutembelea baadhi ya shule, kuendesha mikutano na kushiriki katika kazi za maendeleo ya jamii hasa mashuleni, kutakuwa pia na kongamano la elimu kimkoa lenye lengo la kuangazia kwa mapana changamoto za kielimu mkoani hapo na namna ya kuzitatua. Maadhimisho haya yanatarajia kufunguliwa na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora tarehe 25 Aprili 2022 na yatafungwa na Mheshimiwa Waziri wa OR-TAMISEMI tarehe 29 Aprili 2022.

 

Mkoa wa Tabora umechaguliwa kufanyiwa maadhimisho ya Juma la Elimu kwa lengo la kuungana na wenyeji kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kuhamasisha upatikanaji wa elimu bora kwa watoto wote. Tunatambua juhudi mbalimbali zinazoendelea mkoani hapo kwa lengo la kufanikisha upatikanaji wa elimu bora kwa wote lakini si vibaya pia na TEN/MET kama mtandao wa elimu wa kitaifa kushirikiana pamoja nao ili kuongeza nguvu zaidi na kufikia malengo.

Tafadhali pakua taarifa yote hapa.