Kulingana na lengo la kuweka uwazi na ufuataji wa kanuni za kitaifa (CAP.56) 2 kifungu cha 13 (a) and (b), Tanzania Education Network/Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) inawataarifu kuwa bajeti ya shirika kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli zake kwa mwaka 2019/2020 ni Shilingi za Kitanzania 2,045,080,856/=.

Shirika limepokea kiasi cha Shilingi za Kitanzania 942,005,235.50 ambapo Shilingi   734,824,286.00 zimepokelewa kutoka Shirika la Maendeleo la Sweden (Sida)  kama sehemu ya mkataba wa ushirika kati ya TEN/MET na Sida katika kufadhili Mpango Mkakati wa miaka 5 (2018 – 2022); na Shilingi  207,180,949.50 zimepokelewa kutoka Shirika la Oxfam IBIS ikiwa ni sehemu ya mkataba wa miaka miwili (2020 – 2021) wa ushirika kati ya TEN/MET na Oxfam IBIS chini ya ufadhili wa Ubia wa Elimu Duniani (GPE).

TEN/MET ni shirika lisilo la kiserikali linaloundwa na mashirika wanachama ambayo ni asasi za kiraia zinazoshughulika na kazi za elimu Tanzania bara . Shirika limesajiriwa nchini chini ya Sheria ya Mashirika yasiyo ya kiserikali ya mwaka 2002 ikiwa na namba ya usajiri 00NGO/00008049.

Malengo makuu katika Mpango Mkakati wa TEN/MET wa 2018 – 2022 ni kujenga uwezo wa taasisi, kuratibu mtandao imara wa   kitaifa wa elimu, kuwajengea wanachama uwezo wa kuleta mabadiliko chanya katika sekta elimu, kufanya tafiti   kwa ajili ya mfumo bora wa elimu Tanzania na kufanya kampeni endelevu juu ya utoaji wa elimu bora nchini. Hii ni pamoja kuchangia dira ya taifa 2025 na malengo ya Maendeleo Endelevu (2030).

kupata nakala kwa kiswahili na kingereza:
Taarifa kwa Uma