NAMBA ZA SIMU KWA AJILI YA JAMII KUWASILISHA TAARIFA ZA UKATILI WAKIJINSIA NA UKATILI DHIDI YA WATOTO
UTANGULIZI;Mojawapo ya changamoto katika kupambana na ukatili wa kijinsia na Ukatili dhidi ya watoto ni kuchelewa kwa taarifa ambazo jamii inazifahamu.Wataalamu Wa Wizara za Kisekta wameendelea kutoa mchango wao kwa kutoa namba za simu ili Jamii ipate wepesi zaidi wakutoa taarifa sambambana kutumia namba y akitaifa ya 116 ya CSEMA inayotoa huduma bila malipo saa 24 kila siku.Namba hizi zitachochea Hamasa na kasi ya uwasilishaji taarifa za viashiria vya ukatili au za matukio ya ukatili.
Ikumbukwe, Serikali inatekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili kwa Wanawake na Watoto wa mwaka 2017/18-Juni, 2022. Aidha, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa Ushirikiano na Wizara za Kisekta itaendelea kuhuisha na kuongeza namba za simu za Wilaya, Halmashauri hadi Kata ili huduma iwe karibu zaidi na jamii.
Tafadhali pakua orodha kamili ya namba za simu hapa