Maadhimisho ya Juma la elimu (GAWE) ni tukio la alama kwa mashirika yasiyokuwa ya kiselikali (CSOs) yanayojushughulisha na elimu. Maadhimisho haya yalianza mara baada ya Mkutano Mkuu wa pili wa kiulimwengu ambao ulifanyika Dakar Senegal mwaka 2000. Kila nchi hufanya maadhimisho hayo katika wiki iliyopangwa na Global Campaign for Education (GCE). Ujumbe/Kauli Mbiu inayotolewa kila mwaka Kimataifa huwa ni ujumbe unaolenga jambo muhimu linalotakiwa kushughulikiwa katika elimu kwa mwaka huo wote na kwa nchi zote, lakini hutolewa nafasi ya kuihuisha kaulimbiu/ujumbe huo kulingana na hali halisi ya nchi husika.

Kwa mwaka huu, TEN/MET inategemea  kuadhimisha Juma la Elimu kama ilivyoada kwa miako zaidi ya 15 ambayo yatafanyika mkoani Mara wilaya ya Rorya kuanzia tarehe 31/05 hadi  tarehe 04/06/2021. Kauli mbiu katika ngazi ya kimataifa ni “UWEKEZAJI KATIKA ELIMU” Sauti Billion Moja kwa ajili ya Elimu, sauti hizo zikihusianishwa na sauti za watoto Billioni moja duniani kote waliokosa elimu kutokana na janga  la KORONA hivyo kuathiri utimizaji wa Malengo ya Maendeleo endelevu hasa lengo nambari  nne (4 ).

Kamati ya Maandalizi ya TEN/MET imeamua kauli mbiu kwa Tanzania iwe ni: “Uwekezaji katika mifumo ya Elimu kwa  Maendeleo  Endelevu”.

Kwa taarifa kamili bofya hapa. Pia unaweza kuangalia hapa.

Unaweza pia kufuatilia kupitia mitandao ya kijamii kwa ‘hashtags’ zifuatazo;

#GAWE2021 na #TUKUTANERORYA