TEN/MET imefanikiwa kufanya utafiti ili kubaini ufanisi, changamoto na uwezo wa vituo vya elimu kwa njia mbadala (alternative education pathways) vinavyoweza kumuandaa na kumsaidia mtoto wa kike aliyelazimika kuacha shule kwa sababu ya ujauzito ili kuweza kutimiza ndoto zake kimaisha. Kulingana na utafiti huu, tumefahamishwa kuwa;

  1. Vituo vingi vinavyotoa elimu kwa njia mbadala vinapatikana maeneo ya mjini na sio vijijini, hivyo watoto wengi waishio vijijini hukosa fursa ya kujiunga.
  2. Pia vituo hivi ili kujiunga kuna gharama ambayo mwanafunzi pamoja na mzazi/mlezi wake lazima wa ghramie ikiwemo, ada, malazi, chakula, usafiri, sare za shule na mengineyo. Hii hupelekea watoto wengi wanaotoka kwenye mazingira magumu ya kimaisha kushindwa kujiunga na vituo hivi.
  3. Hatuna sheria ama sera mahususi inayoongelea mtoto akipata ujauzito akiwa shuleni anatakiwa kufukuzwa shule. Uachishwaji wa shule umekuwa ni mapokeo na tafsiri ya Sheria ya Elimu 1978 iliyofanyiwa marekebisho 2002- kifungu cha sheria namba 4.

Kufuatia utafiti huu, TEN/MET iliandaa mkutano (Caucus) ya siku mbili  kuanzia tarehe 25 hadi 26 Ogasti ili kujadili kwa kina kwa pamoja namna ya kutumia tafiti hizi ili kutoa mapendekezo ya pamoja kwa serikali.

Baada ya mkutano, Mratibu wa Taifa wa TEN/MET alikutana na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali hapa nchini ili kuwaeleza yalijiri katika mkutano huu.

Tafadhali pakua maelezo yote kutoka  hapa.