WANAFUNZI 47,305 WA MWAKA WA KWANZA WAPANGIWA MIKOPO
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo imetangaza orodha ya Awamu ya Kwanza yenye wanafunzi 47,305 wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 150.03 bilioni kwa mwaka wa masomo 2020/2021 unaotarajiwa kuanzia wiki ijayo. Akitangaza orodha hiyo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru amesema kuwa kati ya wanafunzi…