Waraka wa Elimu Na. 2 wa Mwaka 2021 kuhusu urejeshwaji shuleni wa wanafunzi waliokatiza masomo katika elimu ya msingi na sekondari kutokana na sababu mbalimbali
Kupitia waraka huu, Serikali inatoa fursa kwa wanafunzi wanaoacha shule kutokana na sababu mbalimbali kurejea katika mfumo rasmi wa elimu. Fursa hiyo itajumuisha wanafunzi wanaokatiza masomo kutokana na ujauzito ambapo wataruhusiwa kukamilisha mzunguko wa elimu yao katika mfumo rasmi. Tafadhali pakua waraka huo kupitia hapa