TAARIFA KWA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGOs) KUHUSU MFUMO MPYA WA MALIPO KWA NJIA YA MTANDAO
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) anapenda kuyajulisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Umma kwa ujumla kuwa ulipaji wa ada mbalimbali za NGOs umeanza kufanyika kupitia Mfumo wa Malipo ya Serikali wa Kimtandao (Government Electronic Payment Gateway). Utaratibu huu mpya wa malipo unapatikana kupitia Tovuti ya Wizara na Idara ya Uratibu wa NGOs (www.mcdgc.go.tz…