MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YAPEWA SIKU 30 KUWASILISHA TAARIFA ZA MATUMIZI YA FEDHA NA MIRADI KWA MWAKA 2016 NA 2017
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni miongoni mwa nchi nyingi duniani zinazozingatia misingi ya utawala bora katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku. Misingi ya Utawala bora pamoja na mambo mengine inasisitiza uzingatiaji wa masuala ya uwazi na uwajibikaji katika utendaji kazi wa kila siku jambo ambalo Serikali yetu imekuwa ikilihimiza na kulitekeleza ipasavyo.…