Na Elias Msuya, 25 Februari 2021, Gazeti la Mwananchi

Dar es Salaam. Utafiti wa ukatili kwa wanafunzi ulitotelewa na taasisi ya Haki Elimu umeonesha asilima 87.9 ya wanafunzi wamepata unyanyasaji, ambapo asilimia 90 wasemesema walichapwa viboko.

Akitoa matokeao ya utafiti huo jana Februari 24 Dar es Salaam, mtafiti kiongozi ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Moses Mnzava alisema aslimia 54.9 wanapigwa makofi, asimilia54.7 adhabu nhyingine ambapo walimu ndio wanatajwa kuwa wanyanyasaji zaidi.

“Asilimia 89 wanapata adhabu shule na asilimia 10 wanapata nyumbani. Katika maeneo ya vijijini adhabu ya viboko inatolewa kwa asilimia 37.1 wakati mijini inatolewa kwa asilimia 16.3” alisema Dk. Mnzava.

Kuhusu ukatili wa kisaikolojia, Dk. Mnzava alisema asilimia 69.9 ya watoto wameathiriwa.

“Kati yao, kwa wasichana asilimia 66.1 wapo shule binafsi na asilimia 59.4 wako shule za umma.”Kwa wavulana asilimia 65.4 katika shule binafsi wamenyanyaswa kisaikolojia ikilinganishwa na asilimia 58 ya shule za umma”, amesema.

Alitaja matendo ya unyanyasaji kisaikolojia kuwa pamoja na kugombezwa, kuibiwa , kuvunjiwa vitu , kutukanwa na aibu ya kuwa yatima.”Asilimia 81.7 walisema wamenyanyaswa shule, asilimia 15.8 nyumbani na asilimia 2.5 walisema njiani. Kuhusu unyanyasaji wa ngono, amesema katika shule za umma upo kwa asilimia 17 wakati shule binafsi asilimia 14.

“Kwa wasichana waliofanyiwa ukatili ni asilimia 19(shule za umma), asilimia 14.7 shule binafsi na wavulana”, alisema.Alitaja matendo ya ukatili wa ngono kuwa pamoja na maneno ya kimpenzi, watoto kuongweshwa picha za ngono, kufanyishwa mapenzi, kushikwa shikwa kimapenzi.

Akitoa maoni yake kwa utafiti huo, Dk. Mnzava alisema ameishauri Serikali kuweka washauri nasaha shuleni watakaokuwa wakisikiliza malalamiko ya wanafunzi.
Utafiti huo ulionfanywa mwaka 2019 hadi 2020 umehusishwa wilaya 32 katika mikoa 16 nchini ambpo wanafunzi wa shule 128(64 za msingi na 64 za serikali) walihojiwa. Mikoa hiyo ni pamoja na Mwanza, Mara, Shinyanga, Kigoma, Njombe, Katavi, Songwa, Lindi, Ruvuma, Pwani, Tanga, Dodoma, Singida, Kilimanjaro, Manyara na Arusha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu, Dk. John Kalage alisema kutoka na malalamiko ya unyanyasaji wa wanafunzi, Serikali inapaswa kupitia upya kanuni na miongozo kuhusu viboko ili isitumike kuwa chanzo cha ukatili.

“Serikali ihakikishe shule zote zinakuwa na wataalamu wa ushauri elekezi. Tunapendekeza pia kuboresha sera na sheria hasa Sheria ya Elimu ya 1978 na marejeo yake ya mwaka 2002 na kanuni za utoaji wa viboko shuleni”, alisema Dk. Kalage.

Pia alisema kuna haja ya Serikali kutoa tafsiri halisi ya unyanyasaji na ukatili, kwani kumekuwa na tafsiri nyingi zinazo kwamisha uzuiaji wa tatizo hilo.
Akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa Elimu. Maimuna Amour kutoka Wizara ya Elimu alisema kwa sasa Serikali inalifanyia kazi pendekezo ka kupitia kanuni na miongozo ya uchapaji viboko.

“Kwa sasa suala la viboko iko pale pale, ila tunafanyia mapitio upya ili ijulikane nani anayetakiwa kuchapa, viboko vingapi na ni kosa gani na limefanywa mara ngapi”, alisema Maimuma.

Alisema serikali inatafakari uwezekano wa kuweka washauri na wanasihi kila shule watakaosikiliza matatizo ya wanafunzi yakiwemo ya unyanyasaji na kuyapatia ufumbuzi wa kudumu.