Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001 inaweka msing wa uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini na kuweka mazingira wezeshi ya utendaji kazi wa Mashirika hayo kwa kutoa maana ya Shirika Lisilo la Kiserikali, kuainisha vyombo vya usimamizi vya Mashirika na kuweka utaratibu wa kusajili Mashirika. Sera hii ndiyo msing wa kutungwa kwa Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24/2002

Mwongozo huu utasaidia kuweka mazingira wezeshi kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, kuimarisha uwazi na uwajibikaji na kuimarisha ushirikiano katika utendaji na uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali baina ya Wizara yenye dhamana na Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Wizara, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mtaa, Sekta Binafsi na Mashirika yenyewe katika kufanya shughuli za maendeleo.

Utekelezaji wa Mwongozo huu utaenda pamoja na utekelezaji wa Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005 na mwaka 2019 na Kanuni zake, katika kusimamia utendaji na ufuatiliaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika Sekta ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

Serikali inaamini kuwa mwongozo huu utaimarisha mazingira ya utendaji kazi kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili yaweze kutoa mchango wao kikamilifu katika maendeleo ya nchi.

Dkt J.K. Jingu
KATIBU MKUU
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
(MAENDELO YA JAMII)

Pakua au soma zaidi; Muongozo wa NGOs